NI KWA LENGO LA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MKOPO WA ASILIMIA KUMI
Manispaa ya Kinondoni imepokea ujumbe wa watu tisa kutoka Halmashauri ya Ruangwa kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa shughuli za Serikali hasa utekelezaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vijana walemavu na wanawake.
Ujumbe huo uliohusisha wataalamu kutoka Idara ya maendeleo ya Jamii, Uchumi, Sheria, Utawala, Ukaguzi wa ndani na Tehama imepata fursa pia ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya POS ikiwa ni pamoja na kutembelea vikundi vilivyopata mikopo na kujionea wanavyotekeleza majukumu yao na suala la urejeshaji wa mikopo hiyo.
Ruangwa imefurahishwa na elimu waliyoipata ya utekelezaji wa mikopo ya asilimia kumi, matumizi ya POS katika kukusanya mapato na jinsi ya kutatua changamoto zao.
Vikundi vilivyotembelewa ni kikundi cha ufugaji wa kuku kiitwacho MUGALS, kikundi cha utengenezaji wa juisi kiitwacho EMILOTS na kikundi cha kutengeneza sabuni kiitwacho POWER VIJANA vyote kutoka Kata ya Mwananyamala.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.