Akipokea msaada huo kutoka kwa Mkurugenzi wa IST Dr. Mark Hardeman, Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe.Benjamini Sita amesema samani hizi zimekuja wakati ambao Serikali yetu ya awamu ya tano inasisitiza ubora wa miundombinu ya elimu, inayoenda sambamba na ushirikiano wa kielimu baina ya shule na shule kwa lengo la kukuza ujuzi katika kufundisha.
Amesema suala la elimu nchini Tanzania limechukua sura ya kipekee hali inayopelekea viongozi kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanaendana na sera ya elimu bora na kubainisha kuwa Kinondoni tayari wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanatekeleza upatikanaji wa elimu bora na sio bora elimu.
"Katika kuhakikisha tunaendana na kasi ya Mhe. Rais tunatakiwa kuwa wabunifu kila iitwapo leo, leo hii tumepata samani kwa ajili ya shule zetu mbili za Mbweni Teta na Kigogo pamoja na vitabu zaidi ya boksi 44 na tumefanikiwa kupata vifaa hivi kwa kuwa na ushirikiano mzuri na wenzetu wa International School of Tanganyika, hata hivyo tunarajia kupokea vifaa vingi zaidi." Ameongeza Meya.
Aidha Msitahiki Meya amesema kuwa upo mfumo mpya ambao anatarajia kuutambulisha hivi karibuni ambao utakuwa chachu ya mafanikio ya elimu kwa Manispaa yake ambacho kitaweza kuinufaisha Nchi kwa ujumla.
Naye Dr. Mark Hardeman kutoka International School of Tanganyika amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya Taasisi yake na Manispaa ya Kinondoni ni wa kipekee sana na ameahidi kudumisha na kunufaisha sekta mbalimbali zilizopo na zitakazobuniwa wakati wowote.
Kadhalika Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Kinondoni Mwl. Leonard Msigwa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ameishukuru Taasisi hiyo ya shule kwa kuonesha ushirikiano wenye manufaa zaidi tena kwa mda muafaka .
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.