Timu ya mpira wa Pete ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejiweka katika mazingira mazuri baada ya ushindi wa leo dhidi ya Tunduma.
Katika mwendelezo wa mechi za mashindano ya SHIMISEMITA zinazorindima jijini Dodoma, Timu ya mpira wa Pete ya Kinondoni imewaadhibu wenzao wa Halmashauri ya Tunduma magoli 12-5 na kufanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora .
Nahodha wa kikosi cha watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mfariji Bukusi ametamba kuwa kikosi kipo imara na kitazidi kupambana kila mechi Ili kuipeperusha vema bendera ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
"Timu yetu imekuwa na mwendelezo mzuri wa ushindi, na ushindi wetu wa leo umetusaidia kusonga mbele katika hatua ya 16 bora". Ameongeza Mfariji.
Aidha, wachezaji wa mpira wa Pete wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, wamesema kuwa kuingia katika hatua ya 16 bora kumefungua njia kwa timu ya mpira wa miguu ambayo nayo inahitaji ushindi dhidi ya Handeni hapo kesho Ili kuingia hatua kama hiyo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.