Akipokea chuo hiko kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la Goodneighbours, Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamin Sitta amesema chuo hiko kimekuja wakati mwafaka kwani Serikali inahitaji nguvu kazi kwa vijana ili kwa pamoja tuweze kusukuma gurudumu katika kuhakikisha sera ya nchi ya uchumi wa Kati wa viwanda inatekelezwa na viwanda hivyo vinaendeshwa.
Amesema kunapopatikana fursa hizi ni lazima nguvu kubwa ielekezwe kwa vijana wetu katika kuhakikisha elimu hiyo sahihi inatolewa ili kuendana na kasi ya Serikali yetu yenye sera ya uchumi wa Kati wa viwanda inayohitaji vijana wenye ujuzi katika kuviendesha viwanda hivyo.
Awali alipozungumza Mkurugenzi mkuu wa shirika la Good neighbours Bw Hunggoo Ann amesema, wanaamini Kinondoni itaendeleza lengo la kujengwa kwa chuo hiko ambalo ni kukuza kipato kwa vijana, kuwezesha kukuza vipaji katika fani mbalimbali na kupunguza umasikini kwa kuwapatia ujuzi ambao utaongeza vipato vyao.
Naye Mkuu wa chuo hiko Bw Ignas Kisindo amebainisha fani mbalimbali zinazotolewa katika chuo hiko kuwa ni pamoja na Ufundi umeme wa majumbani, Ushonaji, ICT, Udereva, Ufundi magari na udereva na udereva wa kijiko.
Katika hatua nyingine Meya Sitta ameahidi kuwezesha mikopo ya vifaa wahitimu wanaomaliza masomo katika chuo hiko, ili waweze kujiajiri moja kwa moja.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.