Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo amepokea Apatimenti hizo ikiwa ni baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kimkataba Kati ya Manispaa ya Kinondoni na mwekezaji Osterbay Villa kwa mazungumzo Kati ya pande mbili kutokana na kuondoa kesi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 8 mahakamani.
Aidha kwa mijibu wa makubaliano ya mradi huu wa uwekezaji asilimia 60 ya mapato yatakuwa Chini ya Manispaa ya Kinondoni na asilimia 40 yatakuwa Chini ya Manispaa ya Ubungo.
Amezitaja Apatimenti hizo Kuwa ni zile zilizopo Katika majengo ya 277 MAWENZI RD na 322 RUVU RD.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni mhe Benjamin Kawe sitta amewapongeza wakuu wa wilaya ya Kinondoni na ubungo kwa kufanikisha makubaliano hayo yaliyowezesha kupatikana mapato yatakayotumika kugharamia huduma mbalimbali za kijamii Katika Manispaa zote mbili.
Imeandaliwa na
kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.