NI KATIKA KUTEKELEZA MPANGO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI KUPITIA MFUKO WA WANAWAKE NA VIJANA.
Manispaa ya Kinondoni imekabidhi hundi zenye thamani ya tsh Milioni 200,kwa vikundi takribani 154 vya wajasiriamal ikiwa ni katika kuhakikisha inatekeleza vema mpango wa uwezeshaji kiuchumi wanake na vijana.
Hundi hizo zimekabidhiwa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamini Sitta kwa vikundi vya wanawake na vijana, katika hafla ya mpango wa uwezeshaji kiuchumi kupitia mfuko wa wanawake na vijana iliyofanyika katika viwanja vya ofisi za Manispaa ya Kinondoni.
Amesema mpango huu wa uwezeshaji wanawake na vijana umekuwa ukitekelezwa katika mamlaka za Halmashauri zote nchini na Kinondoni ikiwemo.
Ameongeza kuwa wanufaika wote wa mpango huo wa Mikopo wanatakiwa kuwa makini katika kuhakikisha wanakuwa katika vikundi, na kufanya maendeleo, yatakayowasaidia kujikwamua katika maisha
yao ya sasa na ya badae.
Aidha amewasihi wanavikundi kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kuwasaidia wengine wanapokuwa na uhitaji.
Ametoa wito kwa wanawake na vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujiajiri na kufanya ujasiriamali ili waweze kujikwamua katika changamoto za ajira.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi Patricia Henjewele amesema Manispaa yake imetenga takribani tsh Bilioni 3.8 kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 ambayo ni sawa na asilimia 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mfuko wa wanawake na vijana.
Amesema vikundi hivi vimepitia mchakato sahihi na kufuzu vigezo vyote kwa mujibu wa muongozo wa mikopo na utaratibu uliowekwa katika kutoa mikopo hii.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.