Halmashuri ya Manispaa ya Kinondoni inajivunia kuwa na maendeleo lukuki katika kipindi cha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Jabir Chilumba wakati akiongea katika kongamano la kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru Wilaya ya Kinondoni.
“Hakika Waasisi wetu wamefanya kazi kubwa kutoka awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere hadi awamu hii ya sita ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani tunaona maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali ndani ya Manispaa ya Kinondoni,” amesema Bw. Jabir.
Bw. Jabir amesema kuwa tangu tupate Uhuru Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami zaidi ya kilomita 1000 tofauti na hapo awali Kinondoni ilikuwa na Kilomita 51 tu zilizojengwa kwa kiwango cha lami.
Aidha, Bw. Jabiri amebainisha kuwa katika sekta ya elimu Manispaa ya Kinondoni hapo awali ilikuwa na Shule za Msingi 16 tu za Serikali na sasa kuna Shule za Msingi 186 ikiwa baadhi yake zimejengwa kwa mfumo wa Ghorofa tofauti na hapo awali hazikuwepo kabisa ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Lakini pia Bw. Jabir amebainisha kuwa hapo awali Manispaa ya Kinondoni haikuwa na utaratibu wa kutoa mikopo ya 10% lakini katika kipindi cha miaka 62 ya Uhuru Manispaa ya Kinondoni imeweza kutoa mikopo ya 10% kwa akina Mama, Vijana na Watu wenye Ulemavu ambapo kwa mwaka huu Manispaa imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajiri ya Mikopo.
Pia Bw. Jabir amesema kuwa hapo awali Manispaa ya Kinondoni ilikuwa na vituo vitatu (3) vya kutolea huduma za afya lakini katika kipindi cha miaka 62 ya Uhuru Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kuwa na vituo vya kutolea afya 35 vya Serikali na vituo zaidi ya 100 vya watu binafsi.
Mbali na hayo pia Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa hapo awali Manispaa ya Kinondoni ilikuwa na bajeti ya pato la ndani ilikuwa ni Shilingi Bilioni 9 lakini hivi sasa limeongezeka hadi kufikia kiasi cha Shilingi Bilioni 62.9 kwani mfumo wa ukusanyaji mapato umeboreshwa mara dufu.
Hivyo tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza Nchi kwa weledi na umakini mkubwa ikiwepo kuwajali na kuwafikia wananchi wake.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.