Kuelekea kilele hicho chenye kauli mbiu isemayo "Tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ikolojia" kinachotarajiwa kufanyika Juni 5 mwaka huu, Manispaa ya Kinondoni imeadhimsha kwa kufanya usafi katika fukwe ya Jangwani Beach iliyopo Kata ya Kunduchi.
Zoezi hilo la usafi lililoratibiwa na Diwani wa Viti maalum Mhe Jackline Kweka limefanyika wakati ambapo Kinondoni imeweka mpango mkakati wa kuhakikisha fukwe zinalindwa kwa maslahi mapana ya wananchi kwa kuhakikisha ufukuaji wa taka zilizojifukia katika eneo la fukwe unafanyika ikiwa ni pamoja na kuzisafirisha kwenda dampo.
Amesema Kinondoni imejikita katika kuhakikisha suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi na kwamba kauli mbiu ya mwaka huu ikawe sehemu ya chachu katika kuhakikisha inatekelezeka.
Nae Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira ndugu Shedrack Maximilian amewasihi wananchi wanaoishi maeneo ya fukwe kujijengea utaratibu wa kusafisha maeneo hayo na kuahidi ushirikiano kutoka Manispaa wa utoaji wa vifaa na magari ya kuzolea taka pale ambapo eneo husika litahitaji.
Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali wanatarajiwa kuhudhuria.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.