Manispaa ya Kinondoni kupitia Chuo cha kilimo Malolo imeendesha mafunzo ya siku mbili yenye lengo la kuwezesha Vijana kujiajiri kupitia usindikaji wa mazao ya mbogamboga na matunda.
Akiongea wakati akizindua mafunzo hayo yaliyokutanisha Vijana 20 kutoka kata za pembezoni, Mkuu wa Chuo cha kilimo malolo ambae pia ni Mkuu wa Idara ya kilimo na ushirika Manispaa ya Kinondoni Bw Salehe Hija Amesema mafunzo haya ni fursa nzuri kwa Vijana kuweza kujiajiri kwenye masuala ya ujasiriamali kwa kupitia kuongeza thamani kwenye mazao ya mbogamboga na nafaka.
Amesema mafunzo haya kwasasa yanatolewa bure kabisa kwani yanagharamiwa na Manispaa hivyo amehimiza vijana wengi Zaidi kujitokeza kuweza kupata mafunzo haya ambayo yatakwenda kubadili uchumi wa Vijana kupitia ujasiriamali.
Naye Mratibu wa mafunzo toka Chuo cha Malolo Bi Luciana Msangi Amebainisha mafunzo yatakayotolewa kwa siku hizi mbili kuwa utengenezaji wa tomato source na utengenezaji wa cake.
Chuo cha Malolo kinachomilikiwa n a Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kinatarajia kuanza mafunzo kuhusiana na kilimo, lishe na usindikaji wa mazao ya mbogamboja na nafaka kwa hadhi ya veta.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.