Akifungua mafunzo hayo ya siku moja kwa kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) pamoja na Chuo Cha Utumishi wa Umma(TPSC), Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Khanifa Suleiman amesema ni kwa lengo la kuwajengea uwezo Watendaji anaowaongoza, hali itakayowasaidia kutekeleza majukumu yao katika maadili, misingi imara na weledi utakaoleta Tija kwa Halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa Utumishi wa Umma Sifa yake kuu ni kutoa huduma kwa wananchi na si vinginevyo, hivyo kwa mafunzo haya yaliyohusisha Taasisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU), pamoja na Chuo Cha Utumishi wa Umma(TPSC) yatawajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao kwa urahisi na ufanisi ili kufikia lengo lililokusudiwa kwa weledi.
"Ni muhimu kwa ninyi Watendaji wangu kuwa sehemu ya mafunzo haya, maana elimu huwa haifi, ninaamini mkishiriki vema mtakuwa mmepata maarifa na elimu ya kutosha katika kufanya kazi". Amesema Bi. Hanifa Suleiman.
Akitoa mafunzo ya rushwa kutoka TAKUKURU Bi. Bibie. Msumi amesema mtumishi wa Umma anao wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kanuni zinazomuongoza hivyo ni vema kujiepusha na masuala ya rushwa, kwani anayetoa na kupokea wote niwakosaji na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Naye Bi. Mariam Kuhenga kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma katika kufundisha kwake amesisitiza uwajibikaji unaoambatana na maadili kwa mtumishi na kufafanua mada tano ambazo ni maadili na taratibu za kazi kwa watumishi, masuala kuhusu mtazamo, kukataa mabadiliko chanya, mzunguko wa kazi pamoja na uvumi wa taarifa.
Watendaji waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Maafisa Biashara, Afisa Ugavi na Wachumi.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.