Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeanzisha mfumo wa kanzi data kwa wamachinga utakaosaidia kuwaweka pamoja na kutoa fursa za mbalimbali za kibiashara na kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule katika kongamano la wamachinga Wilaya ya Kinondoni leo Oktoba 28, 2023 lenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo kwa wamachinga hao.
"Mfumo huu wa kanzi data utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatambua wafanyabiashara kwa idadi yao kwenye masoko yote ya Kinondoni kwani mfumo huo utakuwa kwa njia ya kielekroniki ambapo mfanyaniashara atambuliwa kwa sura, biashara anayoifanya na yupo soko lipi," amesema Mhe. Saad.
Mbali na hayo pia Mhe. Saad amengeza kuwa mfumo huo utaisadia kuanzisha Microfinance pamoja na utoaji mikopo ya asilimia kumi kwenye vikundi vya wafanyabiashara ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi ndani ya Manispaa ya Kinondoni na Taifa kwa ujumla.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.