Manispaa ya Kinondoni leo imeadhimisha siku ya mvuvi duniani kwa kutoa zawadi kwa wavuvi washindi wa mashindano ya uvuvi wa samaki zoezi lililodumu kwa takribani masaa kumi na moja (11:00).kuanzia saa 12:00 alfajiri hadi saa 11:00Jioni kwa kuvua samaki kwa washiriki wa soko la Samaki lililopo Msasani jijini Dar Es Salaam.
Zawadi hizo zimetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mh Benjamin Sitta alipokuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya kushindanisha wavuvi hao na kupata washindi watatu kwa vigezo vya wingi wa kilo, kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vilivyopo sokoni hapo
Amesema wakati umefika sasa kwa wavuvi kujitambua kuwa, wanalojukumu kubwa la kuhakikisha wanaendana na kasi iliyopo ya uchumi wa viwanda , kwani wao ndio kundi kubwa linalotakiwa ili viwanda vya samaki viweze kujengwa na vijana wengi kupata ajira.
Ameongeza kuwa zawadi hizi za fedha taslimu zinazotolewa leo ni kuthibitisha uwezo mkubwa walionao vijana hawa walioko kwenye kundi hili la wavuvi katika kushiriki uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha malighafi za kuendesha viwanda vya samaki zinaptikana.
Naye Afisa uvuvi wa Manispaa hiyo Bi. Grace Kakama amesema ni vema wavuvi wakaungana kwa pamoja kuchangamkia fursa za uwezeshaji zinapojitokeza ,pamoja na kuwa wamoja katika vikundi vya ulinzi wa rasilimali za bahari na pwani vilivyoanzishwa chini ya sheria ya uvuvi na. 22 ya mwaka 2003 kwa lengo la kuwaunganisha wavuvi na kuwa wamoja katika kuendeleza sekta ya uvuvi Nchini.
Aidha amewataja washiriki walioshiriki shindano la uvuvi kwa aina za vifaa vilivyotumika na idadi yao kuwa ni ishirini na sita (26),na kilo za samaki zilizopatikana ni 107.7
Amebainisha washindi hao kuwa ni Selemani Marijani aliyepata Kg 24 na kuzawadiwa fedha taslimu tsh 400,000/=, mshindi wa pili ni Zuberi Ayubu aliyepata kg 18 na kuzawadiwa tsh 300,000/= na mshindi wa tatu ni Hamisi Juma aliyepata kg 14.5 na kuzawadiwa tsh 200,000/=.
Maadhimisho haya huadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Novemba, na kwa Manispaa ya Kinondoni yamefanyika soko la Samaki kwa kauli mbiu ya wavuvi wa sokoni hapo isemayo "Uvuvi endelevu wa Jodari kwa Maendeleo ya viwanda. "
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na habari
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.