Akiongea katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kijitonyama, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Stella Msofe amesema siku hii ni muhimu kwa watoto wote na hivyo wanastahili kupata haki sawa bila kuwabagua kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosema" Tutekeleze agenda 2040: Kwa Afrika inayolinda haki za watoto"
Amesema Serikali ya awamu ya sita inatambua umuhimu wa siku ya mtoto wa Afrika na ndio maana inaadhimishwa kwa kaulimbiu yenye lengo la kuwakumbusha wasimamizi wa sera na sheria, wazazi, walezi na jamii yote kwa ujumla kujua wajibu wao katika kulinda na kusimamia haki za watoto.
Amesema "Sisi kama watanzania tunayo sera ya mtoto ya mwaka 2008 ambayo ilipelekea kutungwa kwa sheria yetu ya namba 21 ya mwaka 2009 na sera hii ina vipengele vikuu vitano muhimu ambavyo watoto wanastahili kuvitambua na kuvielewa. Vipengele hivyo ni haki ya mtoto kuishi kabla na baada ya kuzaliwa, haki ya kuendelezwa, haki ya kulindwa, haki ya kushirikishwa na kushiriki pamoja na haki ya kupinga ubaguzi.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Songoro Mnyonge alipokuwa akimkaribisha Katibu Tawala Wilaya amesisitiza umuhimu wa kutambua siku hii ya mtoto wa Afrika na kuwataka wazazi, waalimu na jamii nzima kuhakikisha inazingatia kwa kuwapatia watoto haki zao wanazostahili ikiwa ni pamoja na kuipongeza Manispaa hiyo kwa maandalizi mazuri.
Kadhalika Bi. Khalima Kahema Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni amesema kwa kutambua umuhimu wa siku ya mtoto wa Afrika na kaulimbiu yake, wametenga bajeti kwa ajili hiyo na kuhakikisha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Maadhimisho haya ya siku ya Mtoto wa Afrika hufanyika Juni 16 ya kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine ya Umoja wa Afrika kufanya kumbukizi ya mauaji ya watoto yaliyofanywa na utawala wa makaburu kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.