Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), leo wameadhimisha siku ya Moyo Duniani kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wanachi.
Maadhimisho hayo yaliyoenda kwa kauli mbiu isemayo "Tambua namba yako ya uzito, pressure na Sukari" yamefanyika katika viwanja vya Tanganyika pekers kwa kutoa huduma za kupima uzito, kupima shinikizo la damu, Sukari, kupima moyo pamoja na vipimo vya ECG.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, mratibu katika maadhimisho hayo DR. Omary Mwangaza amesema wameendesha huduma hizi kwani ndio magonjwa yasiyo na dalili zinazoonekana kwa haraka yanayoshambulia nguvu kazi ya Taifa kwa kiwango kikubwa.
Amesema " Kila tarehe 29/09 kila mwaka ni siku ya kuadhimisha ugonjwa wa Moyo duniani, na kwa kauli mbiu hii ya mwaka huu inayotutaka kutambua namba yako ya uzito, pressure na Sukari",ni kaulimbiu shirikishi inayomtaka mwanachi kuchukua hatua kwani magonjwa haya dalili zake hazijitokezi kwa haraka na kusababisha tatizo kuwa kubwa kwa kuchelewa kutibiwa pindi inapompasa mtu kufanya hivyo ". DR.Omary
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Prof. Mohamed Janabi amesema ni vema watanzania wakawa na utaratibu wa kupima afya zao hasa vipimo vya moyo kwani moyo ni kiungo kikubwa katika mwili, hivyo kikiwa na tatizo na afya nzima ya mwili itakuwa na tatizo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Kawe kuadhimisha kwa pamoja siku hii ambapo huduma za vipimo hizo kwa siku ya leo ni bure.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.