Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania Wilaya ya Kinondoni imeanzisha Operesheni "Tokomeza Vinywaji Batili" ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vinywaji visivyo salama kiafya.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule, akizindua operesheni hiyo Juni 20, 2024 alisema, "Wilaya ya Kinondoni pamoja na Mamlaka ya Mapato Kwa pamoja tumekubaliana kuondoa vinywaji batili Kwa hiyo tutapita kwenye maeneo mbalimbali na kukagua vinywaji hivyo na kuwachukulia hatua wale wote wanaouza vinywaji batili."
Naye Meneja Mamlaka ya Mapato Tanzania Wilaya ya Kinondoni, Bwn. Dickson Qamara, aliwasisitiza wafanyabiashara kutumia mashine za kielektronini za EFD na pia kuhakikisha vinywaji wanavyouza vina stempu halali za Mamlaka ya Mapato Tanzania . Aidha wafanyabiashara wameendelea kukumbushwa kuhusiana na kutumia mashine za EFD na kulipa kodi kwa wakati kabla ya Juni 30, 2024.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.