Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeungana na Taasisi za Kiserikali na Taasisi binafsi katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ijulikanayo kama "SabaSaba" ya mwaka 2024. Mingoni mwa shughuli zinazofanyika katika banda la Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na kutoa elimu na kuelezea shughuli zote zinazofanyika katika Manispaa ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utoaji wa leseni za biashara, ukasanyaji wa ushuru wa huduma, ukusanyaji wa ushuru wa mabango, kodi ya ardhi na huduma nyinginezo.
Aidha, Manispaa ya Kinondoni imewapa fursa wajasiriamali wa vikundi mbali mbali kushiriki katika Maonesho haya kwa kuuza bidhaa zao ambapo wamefurahishwa na fursa hiyo na kuongeza kuwa maonesho hayo yatasaidia kuongeza masoko na kukua kibiashara.
Akiongea mjasiriamali Bi. Zaituni Rashid, akiwakilisha kikundi cha Zaradi kinachojihusisha na usindikaji na ukaushaji wa viungo vya chakula amesema, fursa ya kushiriki katika maonesho ya SabaSaba yamepelekea kikundi kukua zaidi. "Kupitia mkopo wa 10% kutoka Manispaa ya Kinondoni umetuwezesha kupata mashine tatu zinazosaidia kuzalisha na kukausha bidhaa zetu na kupelekea kumiliki kiwanda kidogo cha uzalishaji".
Vikundi vingine vinavyoshiriki maonesho hayo kwa Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na Zaradi Group, Sir's Product, Afro Nature, Mpingo Craves, Nnara Group, Viziwi Msasani Group na Vaa Orijino. Kauli Mbiu ya Maonesho ya SabaSaba mwaka 2024 ni "Tanzania ni Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji".
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.