Kinondoni yashika nafasi ya pili katika maadhimisho ya 25, ya maonesho ya wakulima ,wavuvi na Wafugaji maarufu kama Nane nane, yaliyoadhimishiwa mkoani Morogoro yakihusisha Kanda ya Mashariki, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Temeke, na nafasi ya tatu ikienda kwa Manispaa ya Ilala.
Akifunga maonesho hayo, Waziri wa Mifugo Mh Luhaga Mpina amesema lengo la maadhimisho haya pamoja na kauli mbiu yake ni kuipa thamani sekta hii muhimu ya Kilimo, Mifugo na uvuvi ambayo ndio msingi pekee kuelekea kutekeleza sera ya uchumi wa Kati wa viwanda.
Maadhimisho hayo yaliyoenda kwa kauli mbiu isemayo "Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa Maendeleo ya viwanda " yakilenga kutekeleza sera ya Uchumi wa Kati wa viwanda, kwa kanda ya Kati, yameshirikisha Halmashauri za Mkoa wa Pwani, Dar es salaam, Morogoro na Tanga.
Kinondoni tunamuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli katika sera ya Uchumi wa Kati wa viwanda kwa vitendo.
Imeandaliwa na
Kitengo chá Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.