Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeteuliwa kuwa ya mfano katika kutekeleza mfumo wa taarifa unganishi wa ardhi (ILMIS) unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya makazi alipokuwa akiongea na watendaji wa Idara ya Mipangomiji, Ardhi na Uthamini katika ziara yake ya kikazi alioifanya leo kwenye Manispaa hiyo.
Amesema Kinondoni imechaguliwa kuwa ya mfano kujifunza na kutekeleza mfumo huo kutokana na ukubwa wake katika sekta ya Ardhi na wingi wa malalamiko katik sekta hiyo ili yaweze kutatulika kwa urahisi.
"Ni ninyi mtakaofanya twende mbele au tupige Mark time katika kutekeleza mfumo huu kwa kuhifadhi nyaraka za Ardhi "Amesisitiza Naibu Waziri.
Ameainisha faida za mfumo huo wa taarifa unganishi wa Ardhi kuwa ni kwanza ni kuondokana na matumizi ya majalada, upatikanaji wa taarifa za ardhi kwa urahisi, hakutakuwepo na umilikishwaji holela wa ardhi, utasaidia kupunguza kero zitokanazo na upotevu wa nyaraka ,kujua takwimu na idadi za viwanja pamoja na kuwa kituo cha taarifa zihusuzo maswala ya Ardhi kwa wakati wowote.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.