NI BAADA YA KUJENGWA MABWAWA(SWIMING POOL) YA KISASA YATAKAYOTUMIKA KUFUNDISHIA.
Manispaa ya Kinondoni imetakiwa kuhakikisha inatafuta eneo kwa ajili ya kujenga bwawa la kisasa litakalotumika kufundishia vijana wa Kitanzania jinsi ya kuogelea.
Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mh Suleiman Jafo alipokuwa akiongea na uongozi wa Manispaa hiyo, pamoja na waalimu wa shule ya Msingi Oyaterbay.
Amesema Serikali ndio wadau wakubwa wa kuhakikisha michezo inawekewa kipaumbele pamoja na Mazingira mazuri ili iweze kwenda mbele na kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.
Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha imejenga mabwawa makubwa na ya kisasa ili Tanzania iweze kuibua vipaji vya wanamichezo wa michezo hii ya kuogelea.
"Mkuu wa Wilaya nakuagiza kanitafutie pitch nzuri ya kujenga bwawa la kuogelea, sio la makanyanya, litakaloruhusu vijana wetu wapate sehemu ya kufanya hii michezo ya bwawa "Ameagiza Jafo
Naye Wazi wa habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema ni lazima kuhakikisha miundombinu ya michezo nchini Tanzania inaimarishwa kwa kiwango cha juu ili tuweze kufikia malengo ya Kimataifa ya michezo tunayoitaka.
Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutawezesha kuibua vipaji ,na kuvilea ili tuweze kuitangaza nchi yetu kimataifa na kupata medani za ushindi katika michezo hii.
"waogeleaji nchi hii wako wengi, lakini hawana weledi, kwa hiyo tunahitaji kulea hivi vipaji "Amesisitiza Mwakyembe.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi ameahidi kutekeleza agizo la Waziri Jafo kwa kuhakikisha kunapatikana eneo zuri la kujenga bwawa la kuogelea la Kimataifa.
"Sisi tunayo maeneo ya kutosha, kazi tuliyopewa ni kutafuta eneo zuri ambalo litafaa kujenga swimming pool ya kisasa, ya Kimataifa, ili tuweze Kinondoni kuzalisha wanamichezo wengi zaidi,tuko tayari, tunakwenda kujipanga, na ndani ya muda mfupi tutaweza kupata hilo eneo ambalo litafaa kwa ajili ya kwenda kujenga swimming pool ya kisasa "Amebainisha Hapi
Kadhalika Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamin Sitta ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fursa ya wadau watakaowajengea kiwanja kizuri kwa ajili ya mchezo wa kuogelea.
Ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha hili linatekelezeka ndani ya muda mfupi hasa ikizingitiwa michezo si tu kufanya mazoezi, bali pia ni ajira.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.