Kamati ya Afya ya Msingi Wilaya ya Kinondoni ikiwa chini ya Mwenyekiti ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule imewataka Wazazi na Walezi kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano katika vituo vya afya ili kupata chanjo ya Surua na Rubela.
Akiongea katika kikao hicho Febuari 12, 2024 Mhe. Mtambule amesema kuwa ni wajibu wa kila mzazi au mlezi kuhakikisha anampeleka mtoto wake kwenye vituo vitakavyowekwa kwa ajili ya kupatiwa chanjo hiyo ya Surua na Rubela.
“Nichukue fursa hii kuwaomba Wazazi na Walezi wote wenye Watoto kuanzia umri wa miezi tisa hadi kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kuhakikisha wanawapeleka Watoto wao kupatiwa chanjo ya Surua na Rubela kwani kufanya hivyo itasaidia kumlinda mtoto dhidi ya magonjwa hayo,” amesema Mhe. Mtambule.
Mbali na hayo pia Mhe. Mtambule amewataka maafisa afya kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu zaidi juu ya chanjo hiyo ili kuondoa dhana potofu ambayo imekuwa ikijengeka mara kwa mara pindi chanjo hizo zinapoanza kutolewa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.