Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, wadau wa Afya na TAMISEMI leo imezindua rasmi kampeni ya chanjo au matone ya polio kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano itakayoenda kwa siku nne kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 21 Mei mwaka huu.
Akizungungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Shedrack Maximilian amesema, Kinondoni imedhamiria kufikia watoto takribani 156,871 huduma itakayotolewa katika Kata 20 na Mitaa 106 ya Halmashauri hiyo.
Ndugu Shedrack amesema Kinondoni kupitia vituo vyake vya Afya 69, pamoja na huduma tembezi, itapita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha lengo kusudiwa linafikiwa na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikisha suala hilo lenye tija kwa familia na Taifa kwa ujumla.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Ndg Samwel Lizer amesema lengo ni kuchanja watoto wote chini ya miaka mitano ili kuwakinga watoto hao dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na ugonjwa huo ikiwemo ulemavu au kifo.
Uzinduzi wa chanjo hiyo inayotolewa bure, umeenda sambamba na na kaulimbiu ya Taifa isemayo "Kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza"
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.