Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo alipokutana na wafanyabiashara wa eneo hilo la Mwenge na kuzungumza nao katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.
Amesema kwa kufanya hivyo ni kwenda sambamba na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi inayosisitiza suala zima la uboreshaji wa miundombinu katika nyanja mbalimbali ikiwemo huduma za jamii kwa wamachinga na wafanyabiashara katika shughuli zao za kujipatia kipato na kukuza uchumi wao.
"Sisi tunamuongozo unaoitwa ilani ya Chama cha Mapinduzi, kwenye ilani hiyo inasema wazi kabisa kwa kipindi cha miaka mitano tunaweka mazingira rafiki kabisa kwa wafanyabiashara yakihusisha maeneo ya biashara, mtaji na uhakika wa eneo hivyo hatuna budi kuhakikisha hilo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu linafanikiwa" Amefafanua Chongolo.
Aidha amefafanua kuwa uendelezaji huo utahusisha ujenzi wa maduka ya kati ya kibiashara(min- supermarket), sehemu za mamalishe, maduka ya rejareja, maduka ya spea za magari, saluni, vituo vya tax na bajaji, migahawa, vyoo vya jumuiya pamoja na huduma nyingine.
Kadhalika amewataka wakazi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo la kiwanja1024 kuwa sehemu ya uendelezaji huo kwa kutoa ushirikiano pale inapopasa ili kwa pamoja turahisishe maendeleo yenye tija kwa biashara zetu na Taifa kwa ujumla.
Alipokuwa akiongea mfanyabiashara mmoja kwa niaba ya wengine ameonesha kuupokea mradi huo na kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha unafanikiwa kwa kiwango chenye tija na kilichokusudiwa, na kuiomba serikali iwafikirie pia mara baada ya kukamilika kwake wawe wakwanza kupatiwa maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara.
Imeandaliwa na
Kitengo cha habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.