Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Kamati ya UKIMWI imekuja na mpango mkakati endelevu wa elimu na utoaji wa vipimo vya hiari vya ugonjwa wa UKIMWI ili kurahisisha utoaji wa huduma ya upimaji wa ugonjwa huo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya UKIMWI, ambae pia ni Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Makongo, Mheshimiwa Joseph Rwegasira, katika kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Tatu kilichoketi Juni 10, 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni.
"Kutokana na maazimio tuliyokubaliana katika kikao kilichopita cha Baraza, leo tumekuja na mpango huu wa kugawa vipimo vya kupima UKIMWI kwa Wananchi ili kurahisisha na kuongeza kasi ya upimaji wa ugonjwa huu ndani ya Wilaya yetu ya Kinondoni," alisema Mhe Rwegasila.
Aidha, Mheshimiwa Rwegasira alisema kuwa licha ya Kamati hiyo kuweka nguvu kubwa katika kutoa elimu juu ya ugonjwa huo na ugawaji wa mipira ya kinga (kondomu), kuunda mipango mbalimbali pia amewasihi Wananchi hasa vijana kuwa na utamadumi wa kupima afya zao kila baada ya miezi mitatu ili kujua hali zao na kujiweka pazuri.
Kwa upande wake Mtoa huduma ya Afya kutoka Hospitali ya Magomeni, Bi. Martha Shija, alisema ni vyema Wananchi kujitokeza kuchukua vipimo hivyo katika maeneo yaliyoainishwa na kujipima wao wenyewe kwa hiari.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.