Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikia na Ofisi ya Kamishana wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam leo wametoa hati za kidijitali takribani 300 kwa wananchi wa Kata ya Wazo na Mitaa yake.
Akitoa hati hizo katika Viwanja vya Wazo mkabala na Kituo cha Polisi - Wazo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ambaye pia ni Diwani wa Kata hiyo Mhe. Leonard Manyama amesema zoezi hili ni katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani wa kuwatumikia wananchi kwa weledi na ubora na wakati uliokusudiwa.
Ameeleza kuwa hati zilizotolewa ni za kidijitali ambapo taarifa ya mwananchi aliyepatiwa hati imewekwa katika mfumo unaomwezesha kujulikana au kutambulika au kupatikana kwa urahisi hali itakayoondoa au kuzuia mianya yoyote ya utapeli au udanganyifu.
Amesema "Kinondoni imedhamiria, na hiki tunachokifanya hapa leo ni uzalendo, tumewafuata wananchi wetu kwa kushirikiana na Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam tumezindua zoezi la utoaji hati za kidijitali, lakini pia kwa kufanya hivi ni katika kuadhimisha mwaka mmoja wa mama Samia Suluhu Hassan madarakani" Mhe. Leonard Manyama.
Naye Afisa Ardhi - Mteule wa Manispaa hiyo Ndg. Geofrey Mwamsojo amesema hati hizi zimetolewa kwa wananchi ambao viwanja vyao vimekamilisha taratibu zote ikiwemo urasimishaji.
Zoezi hilo la utoaji wa hati kwa wananchi limeambatana na zoezi la usikilizaji na utatuzi wa kero za wananchi wa Kata ya Wazo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.