Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule Januari 16, 2024 amekutana na Wajumbe wa Kamati ya Afya Msingi ya Wilaya ya Kinondoni ili kuweka mikakati mbalimbali juu ya tahadhari ya magonjwa ya mlipuko.
Katika kikao hicho moja ya mikakati iliyowekwa ni kuongeza kasi ya kufanya usafi kwa maeneo yote ya Manispaa ya Kinondoni kila wiki siku ya Jumamosi.
"Ili tuweze kuepukana na magonjwa ya mlipuko yatupasa kufanya usafi kila mwisho wa wiki siku ya Jumamosi badala ya mwisho wa mwezi na elimu itolewe maeneo yote ndani ya Wilaya yetu," amesema Mhe. Mtambule.
Mhe. Mtambule ameongeza kuwa usafi utashirikisha wadau mbalimbali pamoja na kuonana na Wakandarasi waliopewa maeneo kwa ajili ya kufanya usafi kuona wana changamoto gani ili usafi ufanyike kikamilifu.
Ikumbukwe kuwa kikao hicho ni moja ya maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila aliyoyatoa katika kikao kilichofanyika Januari 15, 2024 na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wataalamu na Watendaji kutoka Wilaya zote 5 za Mkoa huo kujadili swala la usafi na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.