Mjasiriamali wa bidhaa zitokanazo na nafaka ya soya Bi. Esta Mhanga anayeshiriki maonesho ya wakulima (Nane Nane) ni mmoja wa wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 itolewao na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
"Sisi kama wajasiriamali wanawake tumewezeshwa mkopo wa asilimia 10 uliotupa mafanikio makubwa ikiwepo kuongeza uzalishaji, kupata fursa ya maonesho mbalimbali ikiwemo maonesho ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (Saba Saba) 2023 na sasa tumepata fursa ya kushiriki maonesho ya wakulima (Nane Nane)".
Bi. Esta ni mjasiriamali anayewakilisha kikundi cha Eden Products akiwa na bidhaa zitokanazo na nafaka za soya kama maziwa ya soya, unga wa soya, chai ya soya na unga wa lishe.
Ameongeza kuwa, Manispaa imewezesha kikundi kupata mafunzo mkoani Kigoma na kuweza kutanua wigo wa kibiashara.
Matarajio ya kikundi ni kukua kibiashara, kuongeza mauzo na kupata uzoefu wa kutosha kupitia washiriki wengine wa maonesho.
Kauli Mbiu ya maonesho haya mwaka 2023 inasema "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula".
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.