Fursa zitolewazo na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imekuwa ni chachu ya mafanikio kwa vijana wengi.
Agnes Mnuo ni mjasiriamali anayewakilisha kikundi cha VAA Orijino Products wanaojishugulisha na uzalishaji wa bidhaa za ngozi na kutoa elimu juu ya matumizi ya bidhaa za ngozi.
Akizungumza katika maonesho ya wakulima (Nane Nane) anasema, "kupitia mkopo wa asilimia 10 kutoka Manispaa ya Kinondoni tumeweza kutengeneza mtandao mkubwa, tumepanua masoko, tunapata wateja wa kutosha, tumeweza kuongeza uzalishaji na kuagiza bidhaa za kutosha".
Bi. Agnes ameongeza kuwa, Manispaa ya Kinondoni iliwawezesha vijana kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali katika mkoa wa Kigoma ambapo mafunzo hayo yaliwapa elimu ya kutosha pamoja na kuwakutanisha na wajasiriamali wengine na kukuza mtandao wa wajasiriamali nchini.
Aidha, ameongeza kuwa kabla ya fursa kutoka Manispaa ya Kinondoni walikua wanatengeneza bidhaa chache lakini mkopo wa asilimia 10 umewakuza kimtaji na hivyo kuweza kutengeneza viatu vya shule, viatu wa wazi (sandles), mabegi, mikanda, buti, pochi "wallet", mikoba na viatu vya ofisini.
"Tunashukuru kwa sasa tunapata maombi mengi ya kutengeneza bidha zaidi kutoka sehemu mbalimbali na tumetambulika kwa kiasi kikubwa".
Matarajio ya kikundi hiki ni kuwa na kiwanda kikubwa, kuongeza uzalishaji, kuwa na matawi nje ya mkoa wa Dar es Salaam na bidhaa ziende nje ya nchi kwa ajili ya kujitangaza zaidi.
Kauli Mbiu "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula".
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.