Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Uchumi, Afya na Elimu Mheshimiwa Richard Mgana, ameutaka uongozi wa Shule ya Sekondari Makongo iliyopo Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni, kukazia nidhamu na ufaulu kwa Wanafunzi wa Shule hiyo.
Akiwa katika Sekondari ya Makongo wakati wa ziara ya Kamati hiyo Mei 21, 2024 ikiwa ni moja ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo katika Robo ya Tatu, alisema kuwa, "tunataka mabadiliko ya kinidhamu na ufaulu ifikapo Julai 2024." Aliuambia uongozi wa Shule hiyo kuwa, "ziara ijayo tunataka taarifa za matokeo ya mitihani ya majaribio kwa madarasa ya Mitihani ya kitaifa."
Aidha, ameuelekeza uongozi huo, kuwashirikisha wazazi na Bodi ya Shule katika masuala ya kinidhamu kwa wanafunzi watukutu. Hatua hii inafuatia kuwepo kwa ufaulu duni pamoja na utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo. Miradi mingine iliyotembelewa ni Ujenzi wa Madarasa Sita ya Shule ya Sekondari Songoro Mnyonge, Shule ya Msingi Maalum ya Sinza na Shule ya Msingi Michael Urio.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.