Kamati ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI inayoongozwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Joseph Rwegasira Agosti Mosi, 2024 imefanya ziara ya kutembelea kituo cha UNTOLD PLUS kilichopo Kata ya Kijitonyama ili kuona namna wanavyowasaidia watu wanaoishi na UKIMWI.
Akiongea kwenye ziara hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Wazo Bi. Grace Mkumbwa ameipongeza asasi hiyo ya UNTOLD PLUS kwa kuanzisha mradi huo wa kuwawezesha kiuchumi watu wenye Virusi vya UKIMWI.
“Nawapongeza sana asasi hii kwa kua na mradi wenye malengo mazuri na wenye mchango mkubwa kwa raifa letu kwani watu wenye Virusi vya UKIMWI wanapowezeshwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kama batiki, sabuni , dawa za madoa na kusindika vyakula aina mbalimbali ambavyo vinahitaji mtaji mdogo inachangia kwa kiasi kukubwa kuwainua kiuchumi na kukuza pato la taifa letu hongereni sana,” alisema Mhe. Grace.
Nae, Makamu Mkurugenzi wa Kituo cha watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI (UNTOLD PLUS) Bw. Amani Anton Mgeni amesema kituo chao kimekua na utamaduni wa kuwatembelea wagonjwa nyumbani ili kutambua mazingira wanayoishi ili wanapotoa ushauri wajue unawafikia walengwa kwa kiasi gani ili kuharakisha huduma kwa haraka.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.