Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Harold Maruma imetembelea miradi ya maendeleo kwa lengo la kujiridhisha na hatua za utekelezaji zilizofikiwa kiwango cha ubora pamoja na thamani ya fedha katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Maruma amesema usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ni muhimu sana hasa ikizingatiwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inafikisha huduma kwa wananchi kwa kiwango kilichokusudiwa, chenye ubora na kwa wakati.
"Sisi kama Kamati ya siasa ya Wilaya, jukumu letu ni kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa kwa vitendo, na kipaumbele chetu sisi ni wananchi, kwa kuhakikisha wanapatiwa huduma za Afya, Uhumi na Elimu na ndio maana tuko hapa kwa lengo la kujiridhisha hilo na si vinginevyo" Amesema Mhe. Maruma
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Kiwanda cha Mboji Mabwepande, ujenzi wa chumba cha mionzi "Radiology", maabara, Pharmacy na chumba cha kuhifadhia maiti "mortuary" iliyoko Hospitali ya Wilaya ya Mabwepande, ujenzi wa shule ya msingi iliyopo Mtaa wa Kihonzile, ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Tarimo na ukarabati wa Zahanati ya Mbopo.
Ziara hiyo imehusisha Kamati ya siasa ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Katibu Tawala Wilaya, Mstahiki Meya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Kinondoni.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.