Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni Mheshimiwa Nurdin Yusuph imetembelea maeneo ya wazi na yale yenye migogoro kwa lengo la kujiridhisha na hatua za utatuzi wa changamoto zilizofikiwa lakini pia ni kuainisha matumizi yatakayoenda sambamba na utoaji huduma kwa wananchi pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Kamati hiyo iliyohusisha Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Waheshimiwa Madiwani imetembelea eneo la Boko lenye ukubwa wa 6.2716 Ha kuona viwanja vya block 378 na block B, Ujenzi wa mfereji Mbweni kuona maendeleo yake, viwanja 689, 690 na 691 Kunduchi kuona eneo la viwanja vyenye ofa ya DCC pamoja na Ada estate kuona eneo la wazi lililopo.
Akijumuisha ziara hiyo katika kikao cha majumuisho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa Mheshimuwa Nurdin Yusuph amesema ipo haja ya Halmashauri kuweka mpango mkakati wa kuyaainisha na kuyalinda maeneo yote ya wazi ili kuepukana na uvamizi unaoweza kujitokeza na kusababisha usumbufu mkubwa lakini pia ni kwa ajili ya maslahi mapana ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.