Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mwananyamala Mhe. Songoro Mnyonge, leo imekagua miradi mitatu ya maendeleo kwa lengo la kujiridhisha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kukagua hatua za utekelezaji zilizofikiwa.
Akikagua miradi hiyo, Mhe.Songoro amesema kukamilika kwake kwa wakati ndio lengo lililokusudiwa, kwani maeneo haya ya mradi ni ya kimkakati, na wananchi wanahitaji huduma bora na zenye viwango.
"Haya yote ni maeneo ya kimkakati kwa maendeleo ya Halmashauri yetu, hivyo yatupasa kufanya na kupanga mikakati hii ili iendane sambamba na mabadiliko ya jamii yetu."Amesisitiza Mnyonge
Miradi hiyo iliyotembelewa ni mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji taka Mabwepande chini ya mkandarasi CRJE, mradi wa ujenzi wa barabara ya Tegeta nyuki urefu wa km 2.2 unaojengwa na TARURA, kwa kiwango cha lami, na mradi unaojishughulisha na utoaji wa namba za Mitaa (Post Code), ulioko Kijitonyama chini ya Manispaa kwa kushirikiana na TCRA.
Katika hatua nyingine, wajumbe wa kamati wameushukuru uongozi wa Manispaa, kwa uibuaji na utekelezaji mzuri wa miradi ya kimkakati na kuelekeza ufanyikaji mzuri wa maboresho utakaoleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.