Kamati ya Mipango miji na Mazingira ya Manispaa ya Kinondoni imefanya ziara kukagua hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika zoezi zima la upangaji na uboreshaji wa Mazingira unaoendelea katika Manispaa hiyo.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mh Songoro Mnyonge ambae pia ni diwani wa Kata ya Mwananyamala imefanikiwa kutembelea na kukagua zoezi la uwekaji wa anuani za makazi, posti Kodi na daftari la makazi katika Kata ya Hananasifu, Kukagua zoezi la upandaji miti katika barabara ya Morogoro na ujenzi wa barabara ya Makanya yenye urefu wa km 5.1 kwa kiwango cha lami.
Kamati imebaini kwamba baadhi ya vibao vya majina ya mitaa katika eneo la Kisutu vimeng'olewa hivyo imeshauri watendaji kufuatilia suala hilo ili kubaini sababu za wananchi kung'oa vibao hivyo kwani huenda wakawa hawajaridhishwa na majina hayo.
Aidha kamati imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Makanya na kushauri yatengwe maeneo ya kupitisha miundombinu mingine Kama Dawasco ili kuepusha usumbufu wa kubomoa miundombinu ya barabara hapo baadae
Imeandaliwa na
kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.