Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo Mh. Oscar Rwegasila Mkasa, imezuru leo kwa lengo la kufuatilia na kujiridhisha na utekelezaji wa maswala ya afya ya VVU na UKIMWI mahala pa kazi, vituo vya afya na zahanati, pamoja na kujiridhisha na mkakati wa utekelezaji wa afua za lishe inayoenda sambamba na mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI katika jamii husika.
Akifafanua zaidi Mh Oscar amesema ziara hii pia imelenga kutembelea kituo cha Afya Tandale na kupokea taarifa za huduma za afya za CTC, kupokea taarifa za ukusanyaji, usimamizi na utunzaji wa takwimu za UKIMWI, kupokea afua za UKIMWI na lishe na utekelezaji wake kwa wanafunzi na waalimu wa shule ya sekondari ya Salma kikwete.
Awali akisoma taarifa ya huduma za ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi Manispaa ya Kinondoni, kwa kamati hiyo ya Bunge Dr. Neema Mlole amesema Halmashauri ilianza rasmi kutekeleza mpango wa Wizara wa kutoa huduma za upimaji wa VVU/UKIMWI, na magonjwa ya ngono mwaka 2000.
Ameongeza kuwa kufikia 2019, kwa Manispaa ya Kinondoni jumla ya vituo 78, vimeendelea kutoa hudumua hizi zinazojumuisha huduma za ushauri na upimaji wa VVU kwa hiari, huduma ya upimaji kwa ustawishi wa mtoa huduma, pamoja na huduma za ushauri nasaha na upimaji majumbani.
Naye Dr. Emanuel Kazimoto, mganga mfawidhi kituoa cha afya tandale, katika taarifa yake ya hudumaa za kitengo cha CTC, ameainisha changamoto anazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake kuwa ni wateja wengi kutokuwa wazi kwa wenzi wao hali inayopelekea ufuasi wao wa dawa kutokuwa mzuri.
Ziara hiyo iliyohusisha TACAIDS, wataalam kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, TAMISEMI, wakuu wa idara na vitengo, pamoja na wataalam kutoka idara ya afya, ilipata fursa ya kutembelea shule ya sekondari Salma kikwete na kituo cha afya cha Tandale ili kujiridhisha na utekelezaji wake kwa vitendo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.