NI KWA LENGO LA KUWAONGEZEA UELEWA WASHIRIKI KUHUSIANA NA MKAKATI WA NNE WA KITAIFA WA KUPAMBANA NA VVU NA UKIMWI (NMSF IV 2018-2022/2023)
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam, yamelenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya kudhibiti VVU na UKIMWI ya Manispaa hiyo (CMAC), ikiwa ni pamoja na kukumbushana wajibu na majukumu yao katika harakati za mapambano dhidi ya UKIMWI.
Akiongea wakati wa ufunguzi, Mratibu wa kudhibiti UKIMWI upande wa kinga wa Manispaa hiyo(CHAC), Bi Rhobi Gwesso amesema Manispaa imeona ni budi kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Manispaa (CMAC) ili waweze kuwa na elimu sahihi watakayoweza kuisamabaza kwa wananchi katika kata zao, na Katika makundi ambayo wanayawakilisha ili waweze kujiepusha na maambukizi na kukabiliana nayo.
Akitoa ufafanuzi juu ya mkakati wa nne wa kitaifa wa kudhibiti VVU na UKIMWI Mwezeshaji kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania (TACAIDS) Bw Delfinus Kivenule amesema, mkakati huo umeandaliwa ili kutoa miongozo kwa sekta mbalimbali katika kupanga na kutekeleza afua za VVU na UKIMWI pamoja na kutafsiri sera ya Taifa kuhusu VVU na UKIMWI kwa vitendo na kuwaongoza wadau katika mwitikio wa Taifa wa kudhibiti VVU na UKIMWI.
Mada mbalimbali ambazo zimewasilishwa Katika mafunzo hayo ni pamoja na Mkakati wa nne wa taifa wa kudhibiti UKIMWI, Muundo wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ngazi ya Mtaa, Kata na Wilaya, Wajibu na majukumu ya Kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI ngazi yamtaa, Kata na Wilaya (MACS, WMACS NA CMAC) ,
Nyingine ni Uongozi na ubia Katika mwitikio wa VVU, Ukweli kuhusu UKIMWI, kifua kikuu na homa ya ini, mawasiliano kuhusu UKIMWI na tafsiri ya Sheria ya kudhibiti VVU na UKIMWI nchini Tanzania ya mwaka 2008.
Mafunzo hayo yaliyoanza tar 4 -6 mwezi wa pili 2019, yamehusisha Kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI ikiwa ni pamoja na waheshimiwa Wabunge, Mstahiki Meya wa Manispaa, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa, Wajumbe wakaribishwa toka kwenye uwakilishi wa jamii pamoja na wataalam wa Idara mbalimbali za Manispaa.
Imeandaliwa na
kitengo Cha Habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.