Kamati hiyo chini ya Kaimu mwenyekiti ambaye pia ni diwani wa Kata ya Wazo Mhe Leonard Manyama imetembelea Asasi hizo kwa lengo la kujionea utekelezaji wa shughuli zake lakini pia kubadilishana uzoefu kaika masuala yahusuyo afua za VVU na UKIMWI.
Mhe. Manyama amesema dhana nzima ya kubadilishana uzoefu katika masuala haya ndio msingi imara unaoleta ushirikiano utakaojenga Taifa letu hasa ikizingatiwa lengo ni kupunguza maambukizi katika Jamii hali itakayopelekea mwamko katika utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ili kwa pamoja tuweze kusumkuma gurudumu la maendeleo.
"Ushirikiano huu ni mzuri, tunachotakiwa kufanya kama Halmashauri ni kuhakikisha tunaweka misingi madhubuti ya ufuatiliaji wa Asasi hizi ili kujiridhisha na huduma zitolewazo" Ameongeza Mhe.Manyama.
Naye Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Kinondoni Bi Rhobi Gweso alipokuwa akizungumza amesema, Kinondoni imekuwa ikishirikiana na Asasi hizi kwa ukaribu Sana lengo kubwa ikiwa ni kusaidiana kwa pamoja kufikia lengo la Taifa la 95%, 95%,95% la kutokomeza UKIMWI ifikapo 2025.
Asasi zilizotembelewa ni Asasi ya "Care for AIDS" inayojishugulisha na Afua za VVU na UKIMWI, pamoja na Asasi ya "STEPS TANZANIA" iliyojikita zaidi na afua za watumiaji wa dawa za kulevya.
Ziara hiyo imehudhuriwa pia na wakuu wa Idara na vitengo, wawakilishi wa makundi ya dini, vijana, wazee na wenye ulemavu.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.