Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Thadei Massawe imetembelea miradi mitano ya shule za awali, msingi na sekondari kwa lengo la kujiridhisha na ukamilishaji wa vigezo vya usajili pamoja na hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwa ujenzi wa shule za msingi na sekondari.
Akiiongoza kamati hiyo Mhe.Thadei amesema kuboreshwa kwa miundombinu ya elimu ndio msingi imara wa upatikanaji wa elimu iliyo bora, hivyo kama kamati hatuna budi kujiridhisha na swala hilo muhimu kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, unaowataka watanzania kijiajiri kupitia elimu.
"Miundo mbinu ya elimu pamoja na mazingira vikiboreshwa, hakika vijana wetu watapata elimu iliyobora, kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, Serikali yetu ya sasa inathamini sana elimu, na sisi kinondoni tunatekeleza hilo."Ametanabaisha Mhe.Thadei
Aidha kamati wamesisitiza ukaguzi wa mara kwa mara wa taasisi binafsi na shule ili kujiridhisha si tu ubora wake, bali hata elimu inayotolewa pale kwani wataalamu wa elimu wapo na hasa ikizingatiwa jamii imara hujengwa na taasisi imara.
Shule zilizotembelewa ni shule ya awali na msingi Kisanga iliyopo Wazo, Shule ya awali Jubilation iliyopo Bunju, Shule ya awali na Msingi Erastus iliyopo Mabwepande, Shule ya Sekondari crown iliyopo Mbezi beach Makonde, na Shule ya awali na msingi Readers Rabbits iliyopo Msasani.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.