Kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu Manispaa ya Kinondoni imefanya ziara kutembelea miradi ya Maendeleo kwa lengo la kuangalia hatua za utekelezaji zilizofikiwa ikiwa ni pamoja na ubora wake.
Ziara hiyo imefanyika leo chini ya Mwenyekiti wake Mh Thadei Massawe ambae pia ni diwani wa Kata ya Ndugumbi na kufanikiwa kutembelea na kukagua miradi ya elimu pamoja na afya.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa jengo moja la choo chenye matundu 12 katika shule ya msingi Magomeni, na milambo pamoja na Ujenzi wa jengo la huduma za afya ya mama na mtoto katika zahanati ya Madale.
Kamati hiyo pia imepata fursa ya kutembelea kikundi cha wanawake cha Amani ambacho kinanufaika na mikopo ya Halmashauri na kujionea shughuli wanazozifanya.
Aidha kamati imeridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi unaoendelea na kusisitiza kushughulikiwa kwa changamoto zilizopo kwa wakati, zikiwemo huduma za kibenki kusogezwa karibu na wajasiriamali.
Imeandaliwa na
kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.