Kamati ya Huduma za uchumi, afya na elimu Manispaa ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wake Mh Thadei Massawe imefanya ziara kutembelea miradi ya Maendeleo kwa lengo la kukagua hatua ilipofikiwa pamoja na utekelezaji wa maagizo yake.
Kamati hiyo pia ilipata fursa ya kutembelea kiwanda cha mabati cha MMI STEEL kilichoko Mikocheni kuangalia hali ya usafi wa mazingira na uzalishaji wa kiwanda pamoja na kukagua shule za awali ili kuangalia Mazingira yake na utaratibu mzima wa uendeshaji na utendaji wake.
Shule hizo ni Milestone Pre and Primary School iliyoko kunduchi, Redave Pre and Primary school iliyoko mabwepande na Kids Planet iliyoko Mbweni.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.