Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi Mhe. Michael Urio, imekagua miradi ya elimu, afya na masoko kwa lengo la kujiridhisha na hatua za ujenzi zilizofikiwa ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akiwa katika ziara hiyo iliyohusisha wakuu wa idara na vitengo pamoja na waheshimiwa Madiwani, Mhe.Urio alipata fursa ya kuona, kukagua kusikiliza na kuainisha hatua, thamani, ubora na changamoto zilizopo katika miradi hiyo ili ziweze kutatuliwa kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla
Amesema sekta ya elimu, Afya na Uchumi ndio Moyo wa Halmashauri unaobeba shughuli na miradi inayogusa mwananchi moja kwa moja hivyo ni vema kuweka mkakati madhubuti wa ufuatiliaji kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora uliokusudiwa.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa miradi yenye ubora hupelekea kutoa huduma bora kwa wananchi kutakakoimarisha afya na uchumi wao hali itakayoleta uimara na uthabiti katika utekelezaji wa shughuli za Maendeleo.
"Sekta ya Uchumi, Afya na elimu ni sekta inayomgusa mwananchi moja kwa moja, hivyo nilazima tujiridhishe miradi hii inatekelezwa kwa viwango na thamani ya fedha inaonekana ili iweze kutoa huduma bora kwa jamii" Amesisitiza Mhe.Urio
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na zahanati ya Tandale, soko la bwawani, chuo cha veta kilichopo Madale, ujenzi wa choo na Rotary club iliyoanzishwa shule ya sekondari Mtakuja iliyopo Kata ya Kunduchi.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.