Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi Mhe. Michael Urio, imekagua miradi ya elimu, afya na masoko kwa lengo la kujiridhisha na hatua za ujenzi zilizofikiwa ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akiwa katika ziara hiyo iliyohusisha Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Waheshimiwa Madiwani, Mhe. Urio alipata fursa ya kuona, kukagua na kusikiliza changamoto zilizopo katika miradi hiyo ili ziweze kutatuliwa kwa haraka na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
"Kamati tunatoa maelekezo miradi yote tuliyoikagua ya elimu, afya na masoko ikamilike kwa wakati kama tulivyopanga kwa kufuata vigezo vya kiuhandisi (specification) zilizowekwa haswa katika milango na fremu za milango kwa ufuatiliaji na ubora uliokusudiwa". Amesema Urio.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa miradi yenye ubora hupelekea kutoa huduma bora kwa wananchi kutakakoimarisha afya na uchumi wao hali itakayoleta uimara na uthabiti katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni Kituo cha Afya Mbweni Malindi, Soko la Wamachinga Bunju B, Shule ya Sekondari Kunduchi na Shule ya Msingi Michael Urio iliyopo Kata ya Kunduchi, Jimbo la Kawe.
Imeandaliwa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
Manispaa ya Kinondoni,
Julai 28, 2022.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.