Kamati ya fedha na uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Songoro Mnyonge, ambaye pia ni Meya wa Manispaa hiyo, Mei 22, 2024 imefanya ziara ya kutembele maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo ndani ya Manispaa hiyo.
"Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imedhamilia katika mwaka ujao wa fedha kuongeza makusanyo ya mapato yake ya ndani kutokana na miradi ya uwekezaji. Kwa hiyo tunayo maeneo takribani kumi tunataka tuyatumie kwa ajili ya uwekezaji na uwekezaji ambao tumedhamilia kuufanya ni ujenzi Mahoteli na Nyumba za kupangisha". Amesema Mhe. Mnyonge.
Hivyo Mhe. Mnyonge amewataka Wananchi wote wenye nia ya kuwekeza wanakaribishwa kuja kuwekeza katika Manispaa ya Kinondoni. Waje kuwekeza kwenye Nyumba za kupangisha (Apartments) na kwenye Mahoteli kwani Manispaa ya Kinondoni ina maeneo mazuri ya uwekezaji, na maeneo yote yapo sehemu nzuri, maeneo ya ufukweni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.