Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa ya Kinondoni imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kwa lengo la kuangalia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wake.
Kamati hiyo chini ya Kaimu Mwenyekiti, ambaye pia ni Naibu Meya Manispaa ya Kinondoni Mh Manyama Mangalu imetembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa arobaini vinavyojengwa katika shule za Sekondari tisa, ikiwa ni mkakati wa kutatua upungufu Wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari.
Vyumba hivyo vya madarasa vimejengwa katika shule za Sekondari zifuatazo:Wazo vyumba vya madaras (12),Kunduchi vyumba vya madarasa (6),Kigogo vyumba vya madarasa (2), Kijitonyama vyumba vya madarasa (4), Makumbusho vyumba vya madarasa (3), Mabwepande vyumba vya madarasa (4), Makongo vyumba vya madarasa (2), Bunju vyumba vya madarasa (4),na Salma Kikwete vyumba vya madarasa (4).
Ujenzi wa vyumba hivi arobaini katika awamu ya kwanza kwa shule za Sekondari tisa (9) ukikamilika, utakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 160, kwa maana ya kila darasa kuwa na wanafunzi 40.

2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.