NI ILE ILIYOGAWANYWA BAADA YA KUVUNJWA KWA ILIYOKUWA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwananyamala na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songoro Mnyonge, imetembelea miradi iliyogawanywa baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kujiridhisha na uhalali wake.
Mheshimiwa Songoro amesema Manispaa iandae mpango mkakati wa matumizi sahihi ya miradi hiyo inayoenda sambamba na ulinzi pamoja na umiliki wake ili kuepukana na usumbufu unaoweza kutokea hasa uvamizi wa maeneo ya viwanja
Ameongeza kuwa katika mpango mkakati huo utazame pia suala la matumizi litakaloenda sambamba na uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato kwani miradi hiyo pia inaweza kutumika kwa lengo hilo, hasa ikizingatiwa agenda ya Halmashauri ni kukusanya mapato ili iweze kutekeleza shughuli za maendeleo.
Miradi iliyotembelewa ni viwanja, majengo ya uwekezaji yaliyopo Msasani, majengo ya biashara, maeneo ya maegesho ya magari pamoja na gari la kubebea maji safi lililopo matengenezo.
Ziara hiyo imehusisha wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.