Kamati hiyo iliyoongozwa na Naibu Meya wa Manispaa, ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kigogo Mh George Mangalu Manyama imetembelea miradi mitatu ya maendeleo kwa lengo la kujiridhisha ubora unaoenda sambamba na thamani ya fedha iliyotumika.
Katika ziara hiyo iliyohusisha wajumbe wa kamati ambao ni Wah.madiwani, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalam, imekagua mradi wa ujenzi wa kituo kidogo cha afya kigogo, ujenzi wa soko la sinza 11 kijitonyama, na ujenzi wa barabara ya salasala kinzudi kiwango cha lami, yenye urefu km 0.7 inayojengwa na TARURA .
Mh.Mangalu amesema hatua iliyofikiwa miradi hii ni nzuri na ya kuridhisha, inayoonesha mwelekeo wa dhamira ya dhati ya utekelezaji na ukamilishaji wake ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
"Miradi hii inaendelea vizuri, chamsingi ni kwamba juhudi zaidi ziongezeke kwa miradi hii kukamilika, ili wananchi waweze kupata huduma bora na pia ni vyanzo vizuri vya mapato",Amesisitiza Mangalu.
Aidha amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanaitunza na kuithamini miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao, ikiwa ni pamoja na kuwa walinzi wa uchafuzi wa mazingira na kuhakikisha wanaitunza mitaro ili iweze kutumika kwa makusudi kamili.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.