Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoeendana na thamani ya fedha zilizotengwa kwenye miradi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa Agosti 24, 2024, katika ziara iliyofanywa na kamati hiyo ambapo wametembelea miradi mitano iliyopo Jimbo la Kinondoni na Kawe.
Moja ya miradi iliyotembelewa ni Shule ya Msingi ya Richard Mgana ambayo itagharimu Bilioni 1.1 mpaka ukamilisho wake, Stendi ya Mabasi Mwenge iliyogharimu Bilioni 12, Uwanja wa Mpira Mwenge utakaogharimu Bilioni 11.8 mpaka ukamilisho wake, Barabara za Jamirex zilizogharimu Bilioni 1 zenye urefu wa Km 1.07 na Ujenzi wa vyumba 18 na Matundu 33 ya vyoo Shule ya Sekondari Songoro Mnyonge utakaogharimu Bilioni 1.3.
Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Justin Nyamoga amesema Kinondoni ni moja ya Manispaa ya mfano hapa Nchini katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.
"Hakika Kinondoni ni Manispaa ya mfano na kuigwa katika utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Maendeleo hususani miradi ya kimkakati kwani miradi hii ambayo tumeitwmbelea ni miradi bora na imeonesha thamani ya fedha iliyotengwa katika utekelezaji wa miradi kwani imetumika vizuri niwapongeze sana timu nzima ya Manispaa ya Kinondoni," alisema Mhe. Nyamoga.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.