Wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi likiendelea katika siku yake ya kwanza, Viongozi wakuu wastaafu nchini wamewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa.
Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Marais wastaafu, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete walipokuwa wakihesabiwa katika makazi yao ya Kawe na Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamebainisha faida za sensa zikiwemo kuiwezesha Serikali kupanga kwa ufasaha miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe, amewapongeza wakazi wa Kinondoni na Mkoa mzima wa Dar es Salaam kwa kuitikia vizuri zoezi la Sensa linalooendelea.
"Zoezi hili limeanza usiku wa kuamkia leo kwa kuanzia katika makundi maalum. Zoezi linaendelea vizuri, nazidi kuwaomba wakazi wa Kinondoni kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa. Siku bado zipo hivyo, tuendelee," Mheshimiwa Gondwe alisisitiza.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.