Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kubuni miradi ya ziada ili kuepukana na vitendo vya kupokea rushwa. Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Kuizuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bi. Dorothea Mrema, aliyasema hayo wakati akiwa na Maafisa Watendaji Kata, Maafisa Ugani na Maafisa Afya katika kikao kazi Mei 15, 2024 katika ukumbi wa Soko la Magomeni. Aliwaasa watumishi wa Umma kujishughulisha katika shughuli halali za kiuchumi huku wakizingatia Sheria za Utumishi wa Umma.
Alisema, "Mshahara mdogo sio sababu ya mtumishi wa umma kupokea rushwa. Tuanzishe miradi itakayotuingizia vipato nje ya mshahara. Lakini tuhakikishe miradi hiyo haiathiri utendaji kazi wa shughuli za umma."
Aidha, Bi. Mrema aliwaasa watumishi wa umma kuishi kulingana na vipato vyao na kuepuka kuishi maisha zaidi ya vipato vyao.
"Hata tukiongezewa mishahara bila kujitathmini sisi wenyewe bado mishahara haitatosha. Hivyo tuache tamaa na tuishi maisha yanayolingana na vipato vyetu." Bi. Mrema alisema.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.