Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa uwekezaji wenye tija na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye ubora.
Pongezi hizo zilitolewa Aprili 16, 2024 na Mstahiki Meya wa Jiji hilo, Mheshimiwa Prof. Davis Mwamfupe, aliyewaongoza Madiwani na Wataalam katika ziara ya mafunzo ya siku moja ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Ujumbe wa Madiwani hao ulitembelea Kituo cha Mabasi Mwenge na Ujenzi wa uwanja wa Mpira kilichopo Mwenge.
Mstahiki Meya Profesa Mwamfupe alisema, "Binafsi naipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa uwekezaji mkubwa hasa katika mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mwenge sambamba na ujenzi wa uwanja wa mpira. Miradi hii itakuza na kuinua kwa haraka ukusanyaji wa mapato ya Manispaa, hivyo na sisi tunapaswa kuyaiga haya ili kuharakisha maendeleo ya Jiji letu,"
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, alisema, licha kupongeza ujio huo pia alishauri kuwepo na uwekezaji ndani ya Jiji la Dodoma ili kurahisisha ukuaji na ongezeko la ukusanyaji wa mapato.
Nae Afisa Biashara wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Philipo Mwakibete, alishauri Mamlaka hizo mbili kuchangamkia fursa za uwepo wa fainali za kombe la Afika (AFCON) kwa kufanya uwekezaji mkubwa ambao utachangia kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.