Shule ya Sekondari Mzimuni ya Manispaa ya Kinondoni, imepata msaada wa shilingi za Kitanzania milioni 227 sawa na Dola za Kimarekani 98,258 kwa ajili ya uboreshaji mazingira.
Msaada huo ulioshuhudiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, umetiwa saini leo baina ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Hanifa Suleiman Hamza na Balozi wa Japan nchini Mheshimiwa Misawa Yasushi.
Kupitia msaada huo, Sekondari ya Mzimuni itanufaika na ujenzi wa matundu ya vyoo 34.
Kwa muda mrefu, Japan imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini: Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.